Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Shah Mahmood Qureshi amesema kuwa, Taliban inapasa kuelewa kuwa baada ya kuidhibiti Afghanistan itahitajia uungaji mkono na himaya ya jamii ya kimataifa; kwa msingi huo inapasa kuheshimu haki za binadamu na sheria za kimataifa. Qureshi ameeleza hayo katika mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na Waziri mwenzake wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Heiko Maas huko Islamabad, siku moja baada ya vikosi vya majeshi vamizi ya Marekani kuondoka Afghanistan.
Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Heiko Maas alisema kuwa, licha ya Taliban kuahidi kuwa wataunda serikali shirikishi na kuheshimu haki za binadamu tunasubiri kuona iwapo watatekeleza ahadi hiyo au la. Matamshi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan kuhusu kuwepo ushirikiano na kutolewa misaada ya jamii ya kimataifa kwa kundi la Taliban iwapo kundi hilo litaheshimu haki za binadamu yanaonyesha kuwa, Islamabad imeitahadharisha Taliban kuhusu taathira mbaya za utekelezwaji wa siasa na vitendo vitakavyopelekea kukandamizwa haki za raia na jamii.
342/